Hizi ndizo mbinu alizotaja Luizio za kuchukua Ubingwa Simba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi ndizo mbinu alizotaja Luizio za kuchukua Ubingwa Simba

Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio ameendelea kuwatia moyo mashabiki wa Simba na kusema matumaini ya klabu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu bado yapo na anaamini lazima watakuwa mabingwa msimu huu.

Luizio alisema hayo baada ya timu yake kuipiga bao 2 - 1 timu ya African Lyon na kuifanya Simba kurudi tena kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 62 na kuishusha Yanga ambayo ilikuwa kileleni mwa Ligi Kuu.

"Saizi tunajiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo ujao, ukizingatia tunahitaji ubingwa msimu huu kwa hiyo lazima tujiandae vizuri na pia naamini tutashinda mchezo huo, lakini niwashukuru sana mashabiki wa Simba kwani siku zote wanakuja uwanjani bila kukata tamaa, ila nawaomba mashabiki waendelee kuja katika michezo yetu iliyobaki kwa wingi kwani support yao inatupa nguvu zaidi sisi wachezaji, hivyo tunajitaji sana suport yao ili kuchukua ubingwa huu" alisisitiza Luizio

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.