Hili likitokea tu, Msuva anaondoka Yanga - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hili likitokea tu, Msuva anaondoka Yanga

Mfungaji bora wa Yanga na VPL Simon Msuva amesema kuna ofa nyingi zinazomtaka kuondoka kwenye klabu hiyo lakini kwa sasa bado anamkataba na Yanga kwa hiyo suala la yeye kuihama klabu yake lipo mikononi mwa viongozi wa timu pamoja na manager wake.

“Ofa nyingi zimekuja lakini mimi bado nina mkataba na Yanga lakini suala hilo nauachia uongozi wangu pamoja na Yanga  kama Mungu atakua amepanga niondoke nitaondoka kama itakuwa bado basi nitaendelea kuwepo.”

Msuva pia amesema, jeraha alilopata wakati anaitumikia timu yake ilipocheza na Mbeya City lilimrudisha nyuma na kumpunguza makali ya kumshinda mshindi mwenzake wa tuzo ya ufungaji bora ambaye ni Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting.

“Majeraha yamenifanya nishindwe kufunga zaidi na kumzidi mpinzani wangu, nilikua naumia kukosa mechi lakini mechi mwisho ya mwisho nilifosi kwa sababu ya kutaka kujiweka sehemu nzuri mimi na klabu yangu.”

“Simon Msuva anaangaliwa na watu wengi kwa hiyo sioni kama kilichotokea uwachani wakati tunavheza na Mbao ndio sababu ya mimi kushindwa kupata tuzo ya mchezaji bora, refa hakupigwa zaidi ya sisi kumfuata na kudai haki yetu.”

“Mimi ninamalengo ya kushinda tuzo hadi nje ya nchi kwa hiyo sifikirii tuzo za hapa tu nataka kupambana kama Mbwana Samatta na kushinda tuzo nje ya nchi.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.