Haya ndio madai ya Shamsa Ford Kumpokonya Mumewe Duka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Haya ndio madai ya Shamsa Ford Kumpokonya Mumewe Duka

Shamsa Ford na mumewe Chid Mapenzi

DAR ES SALAAM: Raha ya ubuyu ukae kitako usikilizie utamu! Baada ya kudaiwa kumfilisi mumewe, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefungua duka Mitaa ya Mwananyamala, Dar, lakini nyuma yake kuna ubuyu mzito.

Ubuyu wa motomoto unadai kuwa, Shamsa amempokonya mumewe duka hilo kwani badala ya kuuza vitu vya wanaume kama lilivyokuwa awali, sasa anachanganya na vitu vingine huku muda wote akishinda mwenyewe.

Sosi wa ubuyu huo alisema ndugu wa Chid wanalalamika kuwa, Shamsa amekuwa juu ya mumewe kiasi cha kufikia hatua ya kumpokonya duka ambalo awali alisingizia mumewe kukosa kodi hivyo likafungwa.

“Unajua Shamsa ni mjanjamjanja sana. Ndugu wa mume wanalalamika kuwa ndiye aliyemshawishi mumewe wafunge duka la awali kwa kisingizio kuwa kodi ni kubwa, lakini kwa sasa amefungua duka lingine na zamu hii anauza mwenyewe.

“Cha kushangaza ameweka mpaka nguo za kike, tofauti na duka la Chid lilivyokuwa spesho kwa ajili ya nguo za kiume,” alitonya sosi wetu.


Shamsa Ford na mumewe Chid Mapenzi
Sosi huyo aliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa, Shamsa amemfanya mumewe hafurukuti kwani hata akiwa naye kwenye matembezi anambana kiasi kwamba hawezi kujiachia kama alivyokuwa akijiachia zamani.

“Unaambiwa Shamsa anakaba hadi kivuli. Hata wakitoka kwenye matembezi yao, mwanaume hawezi kuthubutu kujichanganya na watu hasa wanawake kwani mwanamama anakaba kila kona. Zamani mshkaji alikuwa anajichanganya, hata ungemkuta na washkaji alikuwa haoni shida, lakini kwa sasa hafurukuti,” alidai sosi huyo ambaye ni shabiki kindakindaki wa mwigizaji huyo.

Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Wikienda, kupitia safu hii ya Ubuyu Ulionyooka lilimsaka Shamsa aliyekiri kuwa na duka lingine na kudai kuwa hajampokonya mumewe bali mume wake ameamua kumpa duka hilo kama zawadi tu ili ajiendeleze, asikae bila kazi kwani huu ni wakati mgumu kiuchumi.

BOFYA HAPA KUMSIKIA SHAMSA

“Mh! watu bwana! Hawajui naongea nini na mume wangu tuwapo chumbani, wanachonga tu. Mume wangu ameamua kunizawadia, nikatae kwa sababu ya maneno? Mbona wameshasema mengi? Mimi nadunda tu,” alisema Shamsa.

SHAMSA AFUNGUKA MENGINE Baada ya kuchoshwa na maneno, Shamsa alifunguka mazito zaidi ambapo alidai kwa sasa amekuwa sugu wa maneno kwani watu walisema atakaa kwenye ndoa miezi miwili tu atatoka, lakini sasa anamaliza mwaka.

“Watu hawajui mimi na mume wangu tulikutana vipi, amewapitia wangapi? Tena wengine wazuri kuliko mimi lakini mbona akanichagua mimi? Alilopanga Mungu, mwanadamu hawezi kupangua, ndoa yangu itadumu miaka mia nane,” alifunguka Shamsa.

AWANANGA MASTAA WENZAKE

Shamsa alienda mbali zaidi na kuwananga mastaa wenzake ambao wamekuwa wakidai kuwa, hawataki kuolewa kwa sasa lakini ukweli ni kwamba ni waongo na hawajapata wa kuwaoa kwani kuolewa si mchezo.

“Kuolewa si mchezo jamani, wapo mastaa wengi unasikia wanasema hawataki kuolewa kwa sasa, ni wanafiki wakubwa na waongo, hakuna asiyetaka ndoa bali hawajatamkiwa, asikwaambie mtu kuolewa si mchezo mimi namshukuru sana Mungu,” alisema Shamsa.

AJIPANGA KUACHA POMBE

“Kutokana na mambo ya ustaa, unakutana na mambo mengi, ndoa yangu itadumu kwa sababu mume wangu si mtu wa mambo mengi, hapendi starehe, hapendi pombe, mimi mwenyewe nimejipanga nimeweza kupunguza pombe na sasa naacha kabisa ili kuinusuru ndoa yangu. Mungu hakika atanisaidia na mfungo umeanza naamini sitarudi tena huko. Wabaya wangu wajipange sana.

“Kila kukicha ni zaidi ya jana kwangu mimi na mume wangu, mahaba tunayopeana kamwe shetani hataingia kwa uwezo wake allah,” alimalizia Shamsa.

NENO LA MHARIRI

Shamsa, kama kweli amejipanga kwa sababu ya maneno ya watu, ajipange kwelikweli na abadili mienendo yote kwani unapofunga ndoa tu, shetani hunyemelea wakati wote ili kukuvuruga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.