Harmonize- Natamani kuwa na mtoto kama wenzangu wa WCB - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize- Natamani kuwa na mtoto kama wenzangu wa WCB

Jina lake limeendelea kutajwa zaidi baada ya kusemekana kwamba yeye ni Baba mtarajiwa kutokana na fununu za ujauzito alionao mpenzi wake ambaye ni Mzungu….. LEO TENA ya CloudsFM imemdaka na kumuuliza maswali haya 10 na akayatolea majibu.

'Natamani kuwa na mtoto kama wenzangu wa WCB lakini kusema ukweli mimi sio baba kijacho kama inavyosemekana'-Harmonize 

'Mimi kama meneja wa Harmonize nilikuwa namshauri atulie tu maana Wolper anampenda ndio ushauri wangu kwake'-Ricardo Momo 

'Kwangu Wolper atabaki kama Mwanamke ambaye alikuwa ananishauri vitu vingi vizuri sina neno naye kabisa'-Harmonize 

'Mwanamke ambaye nataka kuwa naye kwa sasa napenda awe mzuri, mstaarabu kuhusu umri wowote tu sina tatizo'-Harmonize 

'Siko kwenye mahusiano kwa sasa ni kweli nimeachana na Wolper'-Harmonize 

'Kusema ukweli nilikuwa na malengo na Wolper lakini ndio hivyo imeshatokea siko naye tena'-Harmonize 

'Mama yangu alikuwa anajua Wolper ni mpenzi wangu lakini sikuwahi kumtambulisha nyumbani kwetu'-Harmonize 

'Sikwenda kumtambulisha Wolper nyumbani kwetu nilikuwa naenda kwenye show Mtwara'-Harmonize 


'Mimi na mshukuru sana mungu kwasababu account yangu ya youtube kwa mwezi ninalipwa zaidi ya mil 5'-Harmonize 

'Sijasema kuwa Woper amenikosea wala mimi sijamkosea sema tumeachana tu kwa amani'-Harmonize 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.