Hali ya Mchezaji wa Simba Jonas Mkude Baada ya Kupata Ajali iliyoua Shabiki wa Simba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hali ya Mchezaji wa Simba Jonas Mkude Baada ya Kupata Ajali iliyoua Shabiki wa Simba

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo na kupata matibabu kwa ujumla.

Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea jana na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.

Ajali hiyo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuingoza Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika.

Lakini hali yake inaonekana kuimarika na imeelezwa jana alikuwa akilalama sana maumivu lakini sasa ana nafuu.

“Anaendelea vizuri, labda tuangalie kidogo kujua zaidi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.