Fainali ya FA kwa wanawake kuchezwa leo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fainali ya FA kwa wanawake kuchezwa leo

Fainali za kombe la FA kwa upande wa wanawake zinatarajia kuchezwa siku ya leo, kwa kuwa kutanisha klabu ya wanawake ya Manchester City dhidi ya Birmingham City.

Mchezaji bora chipukizi wa tuzo za PFA, Jess Carter, amesema klabu yake ya Birmingham City kamwe hawatawaogopa mabingwa wa ligi klabu ya Manchester City katika mchezo huo.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka,19, aliisaidia klabu yake ya Birmingham kuwatoa Arsenal katika hatua ya robo fainali kabla ya kuingia nusu fainali na kushinda katika mchezo wao dhdi ya Chelsea ambapo mwanadada huyo alikiongoza kikosi chake katika hatua ya mikwaju ya penalties.

Manchester City ndio mabingwa wa mwaka wa FA mwaka 2016 pamoja na kombe la Mabara.

“Hatumuhofii yeyote, hata hao City,” Carter alikiambia chombo cha habari cha BBC. “Tumecheza nao mara kadhaa, Tunafahamu uwezo wao pamoja na mapungufu yao.

“Tunafahamu tupo vizuri na wenye uwezo wa kuleta ushindani na ni timu nzuri kunako ligi sasa tutawaonyesha kila mmoja vile tulivyo.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.