Dogo Janja- Mwanamke Ukinihonga tu nakuacha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja- Mwanamke Ukinihonga tu nakuacha

Msanii Dogo Janja amefunguka na kusema katika maisha yake yeye hajawahi kufikiria kumtegemea mwanamke kuendesha maisha yake bali amekuwa akipambana mwenyewe kupigana na maisha huku akidai endapo mwanamke wake akimuhonga yupo tayari kumuacha.

Dogo Janja alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kusema hajawahi kupenda kufugwa au kuitwa Serengeti boys hivyo yeye anapendeza na kula kwa jasho lake mwenyewe.

"Unajua kuvaa ni kitu kinachotoka damuni, siyo kuvaa vizuri lazima unapata pesa kwa mwanamke 'No' kwanza mimi sijawahi kuamini kupitia pesa ya mwanamke, hata nikiwa na mwanamke akinipa hela huwa namuacha kwa sababu sijawahi kupenda kuingwa king'asti, au kufugwa mimi naamini kula nguvu yangu, naamini kula jasho langu kwa hiyo hilo na kulelewa halipo" alisisitiza Dogo Janja 

Mbali na hilo Dogo Janja alisema kuwa suala la kupendeza ni suala la mtu mwenyewe kwani wapo watu wanapesa nyingi lakini hawapendezi huku wapo vijana wengine ambao hawana pesa hizo lakini wamekuwa wakijipenda na kupendeza. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.