Dogo Janja Aponda Uvaaji wa Davido, Asema Hajui Kupendeza. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja Aponda Uvaaji wa Davido, Asema Hajui Kupendeza.

Rapa Dogo Janja amefunguka na kusema msanii kutoka Nigeria Davido licha ya kuwa na pesa nyingi lakini msanii huyo hajui kabisa kupendeza kwani mara nyingi hata nguo anazovaa ni kama zimetundikwa tu mwilini mwake.

Dogo Janja anasema wapo watu wengine wanapesa nyingi lakini suala la kuvaa kwao ni zero na kumtolea mfano Davido kuwa ni moja ya watu ambao wanapesa nyingi lakini hajui kuvaa na hata nguo akivaa zinakuwa hazimkai vizuri mwilini.

Mbali na hilo Dogo Janja alikwenda mbali na kusema kwa bongo yeye ndiye anakamata nafasi ya kwanza kwa uvaaji kwa wasanii huku akisema msanii mwingine ambaye amekuwa akijitahidi tahidi kwa mitupio kuwa ni G Nako, Jux kwa mbali na Joh Makini.

Janjaro aliendelea kusema kuwa wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakivizia nguo za kutungua Kariako ndiyo maana hawawezi kushindana na yeye kwa kuwa yeye nguo zake anaagiza kutoka nje ndiyo maana anaonekana tofauti na wao katika uvaaji na kupendeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.