Dkt Kikwete: Wakoloni wamechangia umaskini Afrika - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dkt Kikwete: Wakoloni wamechangia umaskini Afrika

Aliyekuwa rais wa Tanzania awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete,amesema koloni za mataifa ya Afrika yamechangia kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ikiwemo kuwanyima elimu waafrika wengi katika maeneo waliyoyatawala.

Dkt Kikwete amesema hayo katika Mkutano wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa Afrika mjini Durban Afrika Kusini, lengo hasa likiwa kutafuta namna za kukuza uchumi wa Afrika.

Rais huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika zimechukua hatua katika kuboresha elimu katika mataifa yao kuanzia shule za chekechea,msingi na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma na kuandika katika kujiletea maendeleo

Ameongeza kuwa nchi zinapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu nchi nyingi zilianzia chini sana na uwekezaji wote huu uliopo sasa katika bara la Afrika umefanyika baada ya nchi hizi kupata uhuru.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.