Darassa afunguka kudorora kwa nyimbo yake mpya ‘Hasara Roho’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Darassa afunguka kudorora kwa nyimbo yake mpya ‘Hasara Roho’

Wimbo wa “Muziki” umesikika sana kwenye masikio ya mashabiki kiasi ambacho inanonekana ni vigumu kwa ‘Hasara Roho’ kupenya kirahisi.

Darassa amefunguka kwa kudai kuwa kazi yake mpya ambayo ameiachia wiki iliyopita aliisikiliza kwa umakini akaona huu ndio muda muafaka wa kuiachia kwa mashabiki lakini wao walitarajia wimbo utakuwa kama ‘Muziki’.

“Kitu ambacho kinatokea ni wimbo wa muziki umewakaa sana na kuusikiliza sana kwa namna moja au nyingine,” amekimbia kipindi cha 255 kwenye XXL cha Clouds FM.

“Mimi mwenyewe nilikaa sana na huu wimbo na kuupima, nikaona kuwa ni project ambayo inafaa kufuata na ikawatosha. Kwa hiyo kwa watu kukaa na kutegemea kuwa uje wimbo kama “Muziki” hiko ndio kitu kinachorudisha sanaa yetu nyuma,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.