Bond wa Wastara atoweka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bond wa Wastara atoweka

DAR ES SALAAM: Baada ya kuachiwa na polisi kufuatia kukaa mahabusu ya Kituo cha Magomeni kwa kuhusishwa na ishu ya ujambazi, msanii wa filamu ambaye pia ni mpenzi wa Wastara Juma, Bond Suleiman, ametoweka mjini, Risasi Mchanganyiko linakupasha.

Mara baada ya kuachiwa, msanii huyo alisema kuwa alikamatwa na polisi kutokana na kuponzwa na rafi ki yake ambaye hata hivyo hakumtaja jina wala namna alivyomhusisha.

Chanzo kilicho karibu na msanii huyo kimeeleza kuwa mara baada ya kuachiwa, ameondoka mjini kiasi kwamba hata kipindi chake katika runinga ya Channel Ten, Action & Cuts hakina mpya zaidi ya kurudiwa matukio ya zamani.

“Yaani watu wanajiuliza Bond ameishia wapi maana hapa mjini hayupo tangu alipoachiwa polisi na
Wastara kusafi ri nje ya nchi kwa wiki kadhaa, hadi amerudi bado haonekani, huenda ameenda kujifi cha sehemu, maana hata simu yake ya mkononi haipatikani siku hizi,” kilisema chanzo.

Ili kujiridhisha, Risasi Mchanganyiko lilifi ka nyumbani kwa Bond alikokuwa akiishi na Wastara maeneo ya Ukonga, lakini hakuwepo na hata simu yake ya mkononi haikuwa hewani. Ili kubaini ukweli wa ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wastara ambaye alisema mwandani wake yupo mikoani akisimamia mashamba yao.

“Ninachojua mimi Bond baada ya mimi kusafi ri yeye alienda mikoani kusimamia mashamba yetu ya mazao na mawasiliano yetu yako vizuri tu kama kawaida, hivyo kama kuna mtu ambaye anajua kitu tofauti na mimi ninavyojua labda aeleze vizuri. “Kuhusu kipindi ni kweli alikiacha tangu mwaka jana mwezi wa saba hashughuliki nacho ila siwezi kueleza kwa nini maana mwenyewe ndiye anajua zaidi,” alisema Wastara.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.