Ben Pol ni Shujaa Kupiga Picha Uchi - Dogo Janja - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ben Pol ni Shujaa Kupiga Picha Uchi - Dogo Janja

Baada ya msanii Ben Pol kupiga picha zenye ukakasi na kuzipost kwenye ukurasa wake wa Instgram rapa Dogo Janja ameibuka na kusema kuwa kitendo alichokifanya Ben Pol ni kitendo cha kishujaa sana kwani wengi hata yeye asingeweza kufanya jambo hilo.

Dogo Janja amesema hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha 5Selekt na kusema jambo hilo alilofanya Ben Pol linahitaji moyo na kusema inawezekana kwa sasa likawa na faida kwa msanii huyo ila athari ya kitendo hicho atakuja kuiona baadaye.

"Labda brother alijiuliza akivaaje atapendeza akaamua asivae kitu tu mbona freshi, lakini mimi sidhani kama nitaweza kufanya jambo kama lile kuwaonyesha watu 'Too much' hapana aisee, vitu kama vile vinaishi milele. unaweza kufanya leo ukapata maslahi lakini kesho kikawa na athari katika maisha yako" alisema Ben Pol

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.