Baba kasema huyo sio ndugu yangu- Harmorapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baba kasema huyo sio ndugu yangu- Harmorapa

Baada ya kijana aliyedai kusafiri kutoka Iringa kuja Dar es salaam kwaajili ya kumtafuta Harmorapa kwa madai ni ndugu yake na baadaye Harmorapa kumkataa, Baba wa Harmorapa amempigia simu mwanaye na kumuondoa shaka kuhusu kijana huyo.

Kijana huyo aitwae Frank Omary amedai aliamua kumtafuta Harmorapa baada ya mama yake kumwambia kwamba  rapa huyo ni ndugu yake ambaye wamechangia baba..

Harmorapa amedai baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo mtandaoni alipigiwa simu na baba yake mzazi.

“Nimetoka kuongea na baba yangu amesema siyo kweli, huyo mtu hamfahamu kabisa,” alisema Harmorapa ambaye yeye ni mtoto wa pili kwa upande wa baba yake. “Baba mwenyewe amemshangaa sana, hata jina la huyo jamaa halijui ndio maana akaniambia kwamba huyo sio ndugu yako,”

Harmorapa amemtaka kijana huyo kutafuta ishu nyingine ya kufanya na kuacha kupoteza muda katika mambo ambayo amedai hayawezi kumsaidia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.