Zlatan Ibrahimovic Kucheza Dhidi ya Everton - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zlatan Ibrahimovic Kucheza Dhidi ya Everton

Ibrahimovic kucheza dhidi ya Everton

Timu ya Manchester United itapigwa jeki kwa kurejea kwa Ander Herrera na Zlatan Ibrahimovic ambao walikuwa wakihudumia marufuku ya muda.

Hata hivyo haijulikani kwa uhakika ikiwa Paul Pogba ambaye alikuwa na jeraha la mguu ataweza kurudi. Juan Mata, Chris Smalling na Phil Jones wako nje, lakini Luke Shaw anatarajiwa kurejea na kujiunga na wenzake.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho kuhusu kupigania kumaliza kati ya nafasi za nne bora amesema " anaenda na hesabu"

"Hadi pale hesabu haitowezekana, tutaendelea kujaribu, na kwa sababu hii ni wiki ambayo haipo na ligi ya Europa, hatuna lolote la kufikiria kuhusu bara Ulaya, kwa hivyo wiki hii ni rahisi kutokana na mtazamo huu"

Meneja wa Everton Ronald Koeman hana wasiwasi wowote wa hivi punde kuhusu ustadi wa wachezaji

Mechi hiyo iko karibu sana kwa mchezaji Morgan Schneiderlin, huku Aaron Lennon, James McCarthy, Ramiro Funes na Seamus Coleman wakiwa na majeraha pia.

Meneja wa Everton Ronald Koeman: " Ni vigumu kwa sasa kwa sababu ya majeraha tuliyoyapata takriban wiki mbili zilizopita"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.