Yanga kupaa angani kuifuata Mbao FC Alhamisi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Yanga kupaa angani kuifuata Mbao FC Alhamisi

YANGA SC imefuta mpango wa kupeleka kikosi chake cha kwanza mjini Dodoma kwa mchezo wa kirafiki, na badala yake kitakwenda moja kwa moja Mwanza kwa ndege kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sporrs Federation (ASFC).

Yanga ilipanga kupeleka kikosi chake cha kwanza mjini Dodoma leo kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Kombaini ya Majeshi ya mkoani humo kesho kuazimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania, lakini sasa kikosi cha pili, maarufu kama Yanga B ndio kimekwenda huko.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo kwamba Yanga B imeondoka asubuhi kwa basi kwenda Dodoma kwa ajili ya mchezo wa kesho Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mkwasa ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga, amesema kwamba kikosi cha kwanza kitaendelea na mazoezi hadi keshokutwa, Alhamisi kitakaposafiri kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo na Mbao FC.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.