Wolper Ampa makavu live Harmorapa! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wolper Ampa makavu live Harmorapa!

JACQUELINE Wolper amefunguka kuwa mwanamuziki chipukizi ambaye hivi sasa amekuwa gumzo mjini, Athuman Omary ‘Harmorapa’ anatia hasira kutokana na kauli zake.

Wolper ambaye ana jina kubwa Bongo Muvi, alisema kinachomuudhi kwa Harmorapa ni kitendo cha mpenzi wake, memba wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumuongelea vizuri lakini yeye anapohojiwa na vyombo vya habari anaponda.
“Jamani yaani kama huna moyo unaweza ukapasuka kwa hasira maana Harmorapa anaudhi sana, wenzie wakimuongelea vizuri yeye anawaongelea vibaya unafi kiri mtu ataacha kukuchukia? Abadilike,” alisema Wolper bila kutaja lini na kauli zipi Harmonize alimuongelea vizuri Harmorapa.
Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha, hivi karibuni Harmonize aliondoka kwa dharau katika Kituo cha EATV baada ya kusikia Harmorapa alikuwepo eneo katika eneo hilo ambalo naye aliitwa kwa ajili ya mahojiano.
Chanzo:GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.