Waziri Mkuu: Olewake atakayekula fedha ya mkulima - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Waziri Mkuu: Olewake atakayekula fedha ya mkulima

Tabora. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema haiwezekani chama cha ushirika kikawa ni sehemu ya watu wachache kufuja fedha za wakulima na yeyote atakayebainika lazima hatua za kisheria zitachukuliwa bila kumuonea mtu.

Majaliwa aliyasema hayo jana alipokutana na kuzungumza na viongozi wa vyama vya ushirika vinavyolima tumbaku mkoani Tabora na kuwaeleza sababu ya Serikali kuivunja Bodi ya Chama Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (Wetcu Ltd).

Majaliwa pia aliwaeleza wajumbe hao sababu kuu ilikuwa ni ufujaji wa fedha uliofanywa na uongozi wa Wetcu Ltd.

Akiwa katika ziara ya siku moja mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema; “Hatua zilizochukuwa zilipaswa kuchukuliwa kwa sababu kulionekana ufujaji wa fedha.”

Alisema kulikuwa na ubabaishaji mkubwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha hivyo ilikuwa ni lazima kufanya uamuzi mgumu ili kuwaokoa wakulima

Majaliwa aliwaambia viongozi hao kuwa uongozi wa Wetcu ulikuwa ukichukua fedha pasipo ridhaa ya vyama vya msingi na kuagiza Coasco ikague miamala ya Wetcu katika Benki ya Exim.

“Ilibainika kuwa waliweka fedha katika akaunti maalumu na kupata faida ya zaidi ya Sh800 milioni, lakini fedha zilizoingizwa kwenye akaunti ni Sh100 milioni tu,” alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.