Watu wangu wote wamenitosa - TID - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Watu wangu wote wamenitosa - TID

Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID Mnyama amefunguka na kusema sasa hivi watu ambao mwanzo walikuwa wakimpa support kwenye muziki na mambo yake mengine wamemtosa na hawampi msaada wowote hivyo kila kitu anapambana mwenyewe. 

TID amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema watu hao wameacha kumpa suport baada ya yeye kuachana na madawa ya kulevya hivyo saizi wao wanamuona yeye ni kama msaliti.

"Saizi kila kitu nafanya mwenyewe hata hao mabrother unaosema washanitosa maana wao walikuwa wanapenda kuona nazidi kuharibika, hivyo toka nimetangaza kuachana na madawa ya kulevya wao wananiona mimi kama 'snitch', lakini hilo halina tatizo kwani mimi mwenyewe niko vizuri ndiyo maana unaweza kuona video hii nimetumia pesa nyingi kuifanya na nimelipa mwenyewe, hii pesa ningesema ninue gari basi ningepata Mark X nyingine lakini nimeamua kuiweka kwenye video ili kuleta ubora zaidi" alisema TID 

TID leo ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Woman' na kusema siku yoyote ataachia video ya ngoma. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.