Wachezaji wanaotakiwa na Conte kutua Chelsea msimu ujao - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wachezaji wanaotakiwa na Conte kutua Chelsea msimu ujao

1.Romelu Lukaku. Alikuwa Chelsea hapo kabla na baadae kocha Jose Mourinho aliamua kumuuza kwenda Everton, sasa ndio anaongoza list ya wachezaji ambao kocha Antonio Conte anawataka. Conte anamtaka Lukaku kuziba nafasi ya Costa kama akiondoka katika klabu hiyo au pia kumpa changamoto Costa, thamani ya Lukaku itakuwa ni zaidi ya £80m.

2.Virgil Van Dijk.Mlinzi huyu wa Southampton amekuwa kwenye rada za vilabu vikubwa kama Chelsea na Manchester United, Chelsea wanaweza kutumia kiasi cha £50m kumnasa mlinzi huyu, Van Dijk amekuwa na majeruhi kuanzia mwezi wa kwanza lakini bado tu vilabu vimemganda pamoja na kuwa majeraha.

3.Claudio Marchisio.Kiungo huyu wa klabu ya Juventus tetesi zinadai anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Chelsea katika kipindi cha kiangazi, Conte amekuwa akivutiwa sana na Marchisio na ni wazi kwamba wako tayari kutumia kiasi cha pesa kama £25m, pamoja na umri wake mkubwa wa miaka 31 lakini anaonekana kuivutia sana klabu ya Chelsea.

4.Alvaro Morata.Morata anahitajika Manchester United pia, ana uwezo mkubwa lakini mara nyingi kocha wake mkuu Zinedine Zidane amekuwa hamtumii katika kikosi cha kwanza. Chelsea wanaweza kutumia pia dili lao la kumuuza Hazard kwenda Real Madrid kama chambo cha kumchukua Morata, mabao 13 aliyoyafunga msimu huu yanawafanya Real Madrid kuweka ngumu kwa yeyote anayemtaka, kwani ukimtaka Morata lazima uwe na kuanzia £65m.

5.Tiemoue Bakayoko.Kiungo wa Fc Monaco na tayari tetesi zinasema Monaco wako tayari kumuuza lakini Chelsea wanaweza kukumbana na upinzani wa vilabu vingine ikiwemo Manchester United, tetesi zinasema Chelsea tayari walishazungumza na wakala wa Bakayoko lakini Monaco hawako tayari kumuuza mchezaji huyo kwa bei chini ya £25m.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.