Waamuzi walaani mwenzao kupigwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Waamuzi walaani mwenzao kupigwa

CHAMA cha Waamuzi Mkoa wa Arusha, kimelaani kitendo cha mashabiki wa Nyota FC kumvamia na kumpa kipondo mwamuzi mwenzao, Frank Mtawanye kikidai kilichofanywa ni uhuni na kitendo kisichowatendea haki waamuzi.

Mwamuzi huyo wa pembeni alikumbana na kipigo hicho wakati wa pambano kati ya Nyota dhidi ya Bodaboda lililopigwa kwenye Uwanja wa Shuile ya Msingi
Mringa zikiwa zimesalia dakika 10 huku matokeo yakiwa bao 1-1.

Mashabiki hao wa Nyota walimvamia mwamuzi huo kwa kumuonyesha kibendera straika wao wakati akielekea kufunga na kuamini timu yao inanyongwa mbele ya wapinzani wao wanatokea Karatu.

Kufuatia kitendo hicho Frat Arusha wameonyeshwa kukerwa na Mwenyekiti wao, Soud Abdi, alisema hakuna haki inayopatikana kwa kuchukua sheria mkononi na kudai kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni na sheria za soka na hata za nchi.

“Tunalaani kitendo hiki na tunatoa onyo kwa wahusika wote yaani klabu zijipime na wajirekebishe, maana hakuna anayejua sheria na kanuni na taratibu za soka zaidi ya mwamuzi na kama anakosea hakuna sheria ya kumpiga bali zifuatwe taratibu za malalamiko yanayoweza kushughulikiwa sio sheria mkononi.”

Mwamuzi huyo alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo kiasi kwa kuwahishwa hospitali ya Mkoa Mount Meru ili kupatiwa matibabu ambayo ilibainika kaumia mbavu na maeneo mengine ya mwili wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.