Tunda Afyatuka Kisa Skendo ya Usagaji. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tunda Afyatuka Kisa Skendo ya Usagaji.

MUUZA nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian amefyatuka kuwa, kamwe hawezi kujihusisha na vitendo vya usagaji kama watu wanavyompakazia na analaani vikali kitendo hicho.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Tunda alisema anawashangaa watu ambao wanampakazia kwamba anajihusisha na usagaji kisa tu kuonekana amepiga picha na mtu mwenye viashiria vya usagaji (tom boy) , wakati amekuwa akipiga nao picha kama watu wa kawaida tu na siyo kwamba ana urafiki nao.

“Miongoni mwa vitu vinavyonikera na sivipendi hata kuvisikia masikioni mwangu ni huo upuuzi kwamba ninajihusisha na usagaji, tatizo watu wanapenda kuongea jambo bila kujua undani wake, inawezekana mtu anavyoniona ni tofauti na uhalisia wa tabia zangu, watu waliona kuna mtu nimepiga naye picha na kuhisi ni msagaji wakati aliniomba tu nipige naye picha,” alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.