Tambwe kukimbilia Uarabuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tambwe kukimbilia Uarabuni

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Amiss Tambwe amesema yuko mbioni kutimkia Uarabuni iwapo atashindwa kusaini mkataba mpya na Yanga.

Mkataba wa sasa wa Tambwe unamalizika Mei 20, hata hivyo, uongozi wa Yanga umepanga kumuongezea mkataba mpya.

Mrundi huyo amesisitiza kuangalia zaidi maslahi na nafasi yake ya kucheza katika timu zote nne zilizoonyesha nia ya kutaka saini yake ambazo tatu ni kutoka Uarabuni pamoja na Yanga.

"Nitaipa kipaumbele Yanga, nitaangalia na maslahi yangu, kwa hapa Tanzania sijafikiria kucheza timu nyingine mbali na Yanga," alisema Mrundi huyo na kuongeza.

"Kuna timu tatu zinanihitaji zinazoshiriki ligi huko Uarabuni, lakini nahitaji kumaliza mkataba wangu na Yanga Mei 20, baada ya hapo nitatoa msimamo wangu," alisema Tambwe.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.