Takwimu zaishusha daraja JKT Ruvu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Takwimu zaishusha daraja JKT Ruvu

Dar es Salaam. JKT Ruvu inasubiri miujiza pekee kuinusuru na janga la kushuka daraja msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

JKT Ruvu inaburuza mkia ikiwa na pointi 23, baada ya kucheza mechi 27 na kusaliwa na mechi tatu mkononi za kuinurusu na balaa la kushuka daraja.

Mbali ya JKT Ruvu, timu nyingine zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja ni Majimaji pointi 26, Toto Africans (26), Ndanda (30), Mbao (30), African Lyon (31), Tanzania Prisons (31), Ruvu Shooting (32) na Mbeya City (32).

Hata hivyo JKT Ruvu ipo kwenye hatari zaidi baada ya kushinda mechi tatu (3) kati ya 27 ikitoka sare mechi 14 sawa na pointi 14 na kufungwa michezo 10.

Akizungumzia uwezekano wa kuinusuru timu hiyo isishuke daraja, mshauri wa benchi la ufundi la Maafande hao, Abdallah Kibaden alisema watapigana hadi hatua ya mwisho.

“Tupo kwenye hatua mbaya ila tutaendelea kucheza michezo iliyobaki ili tuone tutakuwa kwenye mazingira gani, lolote linaweza kutokea, hii ni soka,” alisema Kibadeni.

Kama JKT Ruvu itashinda michezo yake yote iliyobaki ambayo ni dhidi ya Ndanda (Nangwanda), Majimaji (Mabatini) na Toto Africans (CCM Kirumba) itafikisha pointi 32.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.