Snura Kumuanika Laazizi Wake hivi karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura Kumuanika Laazizi Wake hivi karibuni

DAR ES SALAAM: Staa wa mduara Bongo, Snura Mushi ‘Snusexy’ amefunguka kuwa, baada ya ukimya wa muda mrefu na kuzushiwa kila mwanaume, sasa anajipanga kumuanika laazizi wake ili watu wamtambue kwani usumbufu umekuwa ‘too much’.

Snura aliliambia Wikienda kuwa, ishu ya kuambiwa mara anatoka na mtu fulani, mara na Mwarabu ni suala linalomsababishia usumbufu hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani kuna kitu kikubwa anataka kukifanya katika kumtambulisha mwanaume anayetoka naye.

“Soon nitawatambulisha shemeji yao maana naona ni miaka miwili sasa nasingiziwa mambo mengi, mara yule mara huyu lakini wasiwe na wasi kwani kuna kitu kikubwa kinakuja,”  alisema Snura.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.