Sirro: Wenye tuhuma dawa za kulevya wafike kituoni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sirro: Wenye tuhuma dawa za kulevya wafike kituoni

Dar es Salaam. Kamishina wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewataka wote walioitwa polisi ili kuhojiwa kwa tuhuma za dawa za kulevya, wafike kituoni hapo mara moja.

Kamishina Sirro amesema hayo leo (jumatano) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema  ni vyema watu hao wakaripoti ili  kama hawana hatia wasafishwe au wakikutwa na hatia wapelekwe mahakamani kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.

"Niwaombe waliopokea wito wa polisi waje wahojiwe kwa sababu mtu akija mwenyewe inasaidia tofauti na anaposubiri nguvu ya dora kutumika kumkamata ambapo lolote linaweza kutokea hasa kwa yule anayekataa hata kukamatwa." amesema Siro

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.