Sinema za Nje Ziingie Nchini Tupate Changamoto - Mtitu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sinema za Nje Ziingie Nchini Tupate Changamoto - Mtitu

PRODYUZA na muigizaji  wa filamu za Kibongo, William Mtitu,  amefunguka kuwa filamu za nje ziendelee kuingia nchini ila kwa utaratibu unaotakiwa kwa sababu zinatoa changamoto kwa wasanii wa filamu hapa nchini ili waweze kutengeneza kazi zenye ubora.

Akizungumza na Mtandao wa Global Publishers,  Mtitu amesema kuwa hakuna sababu ya kuzipiga marufuku filamu zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi badala yake serikali iweke utaratibu  wa kodi kwa kazi hizo.

“Hakuna sababu ya kukataa filamu za nje zisiuzwe nchini bali kinachotakiwa ni serikali kuzilipisha kodi ili twende sawa pia wasanii wa Bongo tunatakiwa kufanya kazi zilizo na ubora, ubunifu kwani zitauzika tu sokoni,” alisema Mtitu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.