Simon Msuva achimbwa mkwara mzito - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simon Msuva achimbwa mkwara mzito

Simon Msuva wa Yanga.

STRAIKA hatari wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, amemchimba mkwara Simon Msuva wa Yanga kwa kumuambia kuwa, asitarajie kwamba msimu huu atakuwa mfungaji bora kirahisi.

Mussa ameyasema hayo baada ya kufikisha mabao 12 kwenye orodha ya wafungaji wa ligi kuu sawa na Msuva, huku akiweka malengo ya kuongeza mengine matano ili kumuacha mbali Msuva.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mussa alisema: “Nimekuwa nikifanya mazoezi sana binafsi ili kuhakikisha nafikia malengo yangu niliyojiwekea msimu huu ya kuwa mfungaji bora.

“Nataka nifunge mabao 17 kwa msimu huu, nadhani yatatosha kabisa kufikia ndoto zangu na wala simhofii yeyote katika kukatisha ndoto zangu hizo, najua mabeki wa timu pinzani wakikutana na mimi watanikamia sana, nimejipanga kukabiliana nao kwa hali yoyote ile.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.