Simba yawaangukia mashabiki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simba yawaangukia mashabiki

UONGOZI wa klabu ya Simba umeomba radhi mashabiki wao kufuatia matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mchezo wao wa Jumapili iliyopita dhidi ya Kagera Sugar.

Simba ikicheza kwenye Uwanja wa Kaitaba, ilikubali kipigo cha mabao 2-1 na kujikuta ikiteremka mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Akizungumza na mashabiki wa Simba katika tawi la timu hiyo mkoani hapa, Meneja wa klabu hiyo, Mussa Hassan 'Mgosi' alisema hakuna haja ya kutafuta mchawi na kuwataka mashabiki kusahau matokeo hayo na kuangalia michezo ya mbele.

"Ni matokeo ya kuumiza lakini ndio mpira, tunawaomba radhi mashabiki wote ambao wameumizwa na matokeo yetu," alisema Mgosi.

Aidha, Mgosi aliwatoa hofu mahabiki wa timu hiyo na kusema Simba imejipanga kushinda mechi mbili zilizobakia mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mgosi alisema kikosi cha timu hiyo kitapumzika kwa siku tatu mkoani hapa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Aprili 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCm Kirumba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.