Simba yamuundia kamati Bocco - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simba yamuundia kamati Bocco

Bocco aundiwa kamati maalum Simba.

KUTOKANA na rekodi nzuri ya mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco kuitungua Simba kila anapokutana

nayo, benchi la ufundi la Simba chini ya kocha wake, Joseph Omog, limeamua kuunda kamati maalum ya ulinzi kwa ajili ya kumzuia mshambuliaji huyo.

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba, kesho Jumamosi watakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na Azam kwenye pambano la nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Bocco kwenye mechi alizokutana na Simba mpakasasa ameshafanikiwa kuifunga timu hiyo mabao 19 kwenye mashindano yote akiwa ndiye kinara wa ufungaji.

Kocha Msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, raia wa Uganda, ameliambia Championi Ijumaa, kuwa tayari wameunda kamati hiyo wakiwashirikisha mabeki wao wakiongozwa na Juuko Murshid kutengeneza mipango ya kumzuia straika huyo ambaye amekuwa akiwasumbua kila mara.

“Bocco ndiye mchezaji anayetusumbua kila tunapokutana na Azam lakini safari hii tumemuundia kamati maalum ya kuhakikisha

hatufungi wala haleti madhara yoyote yale na tuna uhakika wa kulitimiza hilo kwa sababu wachezaji wameonyesha kutuelewa.

“Ukiangalia rekodi yake kwenye mechi na sisi utajua namaanisha nini, lakini safari
hii hatutarudia makosa tunayoyafanya mara kwa mara na tunaahidi kuwafunga wapinzani wetu kwa ajiliya kujisogeza katika hatua nzuri kwenye kombe hili,”alisema Mayanja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.