Simba Sc Yaipakichapo Rhino 2-0 mechi ya Kirafiki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simba Sc Yaipakichapo Rhino 2-0 mechi ya Kirafiki

SIMBA SC imewapa raha mashabiki wake wa Tabora, baada ya kuilaza timu ya Daraja la Kwanza, Rhino Rangers mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini humo.

Mabao yote ya Simba yalipatikana kipindi cha pili, la kwanza likifungwa na winga Shizza Ramadhani Kichuya kwa penalti na la pili likifungwa na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.

Simba iliwasili Tabora kwa mchezo huo wa kirafiki ikitoka Kanda ya Ziwa Victoria ambako ilikwenda kucheza mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikifungwa moja, sare moja na kushinda moja.

Ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kabla ya kushinda 3-2 dhidi ya Mbao FC na kulazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Hata hivyo, Simba ilipewa pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa na Kagera kutokana na madai ya wapinzani wao kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Peter Manyika, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid/Hamad Juma, Novaty Lufunga, Jonas Mkude, Juma Luizio/Hijja Ugando, Said Ndemla/Frederick Blagnon, Pastory Athahans/Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na Mwinyi Kazimoto/Shiza Kichuya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.