Simba na Toto kufa na kupona Leo Uwanja wa CCM Kirumba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simba na Toto kufa na kupona Leo Uwanja wa CCM Kirumba

LEO Toto Africans inaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kuchezamechi ya Ligi Kuu Bara, kituko ni kwamba ‘makomandoo’ watimu hizo wamekesha wakiulinda uwanja huo wakihofia vitendo vya ushirikina.

Imeelezwa kuwa, kila timu inaogopa kuhujumiwa na wapinzani wao hivyo wakajikuta wote wanalinda uwanja huo usiku wa kuamkia jana Ijumaa.

Championi Jumamosi lilifika uwanjani hapo jana Ijumaa asubuhi saa 2:38 na kuwakuta makomandoo hao wameketi karibu na milango ya kubadilishia nguo huku wakiwa makini muda wote.

Mmoja wa walinzi wa uwanja huo alisema, makomandoo hao waliingia tangu juzi usiku wakitangulia wale wa Toto kisha wakaja wa Simba wakitaka kulinda uwanja.

“Walianza kuja watu wa Toto, baadaye kidogo wakaja Simba, sasa walivyoomba kulinda tukawafungulia na kama
unavyowaona tupo nao hapa, tuliwaruhusu kwani timu zao zinakaribia kucheza,” alisema mlinzi huyo.

Mechi ya Toto na Simba mara nyingi huwa ngumu kwa miaka mitano Simba imeshindwa kuifunga
timu hiyo uwanjani hapo na msimu uliopita zilipokutana zilitoka sare ya bao 1-1.

Kuelekea mchezo huo, Toto imeweka kambi katika Wilaya ya Ukerewe wakati Simba kwa siku tatu mfululizo imefanya mazoezi yake kwenye uwanja huo.

Wakati Simba ikiwania ubingwa huku ikiwa kileleni mwa ligi kuu na pointi 61, Toto ipo katika hatari ya kushuka daraja kwani ina pointi 25 katika nafasi ya 15.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.