Sholo Mwamba amtoa nduki Man fongo studio - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sholo Mwamba amtoa nduki Man fongo studio

Mesen Selekta ajibu kashfa ya kutaka kumpiga changa la macho Manfongo Mil 10 kwa kudai msanii huyo alishindwa kutimiza makubaliano ya kazi iliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano kwa kuhofia kushiriki katika wimbo mmoja na msanii Sholo Mwamba.

Mtayarishaji huyo wa muziki nchini amefunguka kuwa madai ya Manfongo ya kulipwa laki mbili kati ya Million kumi siyo ya kweli na kwamba kampuni hiyo ilitoa milion Sita huku ikitaka wasanii wa nne wa muziki wa Singeli kuimba kwa pamoja katika kazi hiyo kwa makubaliano ya kila msanii kupatiwa milioni moja.

Mesen amedai kuwa hakuwa na makubaliano yoyote na msanii huyo katika kufanya kazi kutoka kampuni ya mawasiliano bali alikubaliana na uongozi wa 'Makers Entertainment'  kumtumia Manfongo katika uandaaji wa wimbo uliotakiwa kuimbwa wakati wa tamasha lililokuwa limendaliwa na kampuni hiyo na baadaye msanii huyo kuitosa kazi hiyo kwa kutotokea studio huku akipuuzia kupokea simu.

"Hivi unawezaje kupewa milioni Kumi ukampatia msanii laki mbili, huo ni ujinga na ninsingeweza kufanya hivyo. Mimi Manfongo sikuwa na makubaliano naye na lile halikuwa tangazo kama anavyodai. Mimi nilipata kazi kutoka kampuni ya simu ambayo ilidhamini show moja ya kuzunguka nchi nzima hivyo walitaka wasanii wafanye kitu kuhusiana na show hiyo lakini wakawa wamependekeza wasanii wanao wataka ndipo nilipokutana na uongozi wa Manfongo kujadili kazi. Baada ya kuanza kusumbuliwa na ile kampuni mbona kazi haitoki Fongo akawa anazingua mara ukipiga simu hapokei ikipokelewa anapokea mke wake lakini tulikuja kugundua kuwa anaogopa kufanya kazi na  Sholo Mwamba" Mesen Selekta.

Hata hivyo Mesen amesema hata baada ya migogoro iliyotokea kati ya Manfongo na Defatality music bado anamuhesabu msanii huyo kama chata wa singeli kwa kuwa ameweza kuwa msanii wa kwanza wa singeli kufanya shoo nje ya nchi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.