Shamsa Ford apasuka uso kisa ugomvi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford apasuka uso kisa ugomvi

Msanii wa filamu Shamsa Ford amepokea kichapo Jumanne hii katika harakati za kuamlia ugomvi wa watu ambao walikuwa wanapigana.

Malkia huyo wa filamu amekutwa na mkasa huo ikiwa ni mwezi mmoja toka aibiwe akaunti yake na Instagram yenye follows M.2.

Muigizaji huyo amedai alipigwa ngumi ya uso katika harakati za kutafuta usalama wa watu hao ambao walikuwa wakipigana.

“Jana kwa moyo mmoja nimeenda kuamlia ugomvi watu wasipigane mwisho wa siku nikaambulia Mimi ngumi..HUYU mtu alishiba sana aiseee ngumi ilikuwa nzito sana..😃😃 niombeeni ndugu zangu panauma,” aliandika Shamsa Instagram.

Kwa sasa muigizaji anaendelea vizuri na matibabu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.