RayVanny na Mpenzi Wake Fahyma Wapata Mtoto. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

RayVanny na Mpenzi Wake Fahyma Wapata Mtoto.

Msanii kutoka WCB Wasafi Raymond 'RayVanny' sasa amekuwa baba ramsi baada ya yeye na mpenzi wake Fahyma kujaliwa mtoto wa kiume ambae wamempa jina la 'Jaydan'. 


Kupitia mtandao wa Instagram Rayvanny ameshare picha na jumbe huu hapa chini:

"Kuna Kuachana, kugombana,kutengana lakini kuacha yote hayo Swala Kubwa Sana Ulilolifanya Ambalo sitoweza kulisahau ni Kunipa @jaydanvanny kwenye maisha yangu. Maana Ungweza Kutoa Mimba lakini Ulikua Na nia njema na mwanao .Wengi walikushauri Utoe wakasema unajiharibia Future wakasema bado mapema lakini haukua tayari kumpoteza Mwanao. @fahyma_ @jaydanvanny We love you son #Youngparents"

Kwa upande wake Fahyma yeye ameandika ujumbe huu " Kiukweli kabisa bado sijamwona wa kufanana na wewe nakupenda sana baby @rayvanny na mwanangu kipenzi @jaydanvanny na mwomba mungu atuvushe salama"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.