Ray C asema sasa ni kazi tu, Mapenzi baadaye - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C asema sasa ni kazi tu, Mapenzi baadaye

Msanii mkongwe wa muziki, Ray C, amedai kwa sasa anapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma na wimbo ‘Mapenzi Matamu’, alikuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu akijaribu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zlimuathiri kwa kiasi kikubwa.

Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa mwenye siha njema, Ray C amedai anachokifikiria kwa sasa katika maisha yake ni muziki na siyo mapenzi.

“Mimi sina mpenzi,” alisema Ray C “Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri,”

Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya Wasafi.Com ya Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Unanimaliza’.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya albamu yake mpya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.