Pogba awajia juu wanaomkosoa na kuhoji dau alilosajiliwa Man United - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Pogba awajia juu wanaomkosoa na kuhoji dau alilosajiliwa Man United

\
Toka atue Manchester United kwa rekodi ya usajili ya dunia, Paul Pogba amekuwa akiongelewa sana haswa kuhusiana na kiasi cha pesa ambacho Manchester United wamemnunua na kiwango anachoonesha.

Hata kabla hajaanza kucheza wengi walisema pesa za kumnunulia Pogba ni bora kununua mshambuliaji ambaye kila wiki anafunga, tabu zaidi ilianza baada ya Pogba kuingia uwanjani japokuwa haoneshi kiwango kibovu sana lakink ameshindwa kufikia kile kiwango walichotaraji mashabiki.

Sio tu mashabiki wa soka bali na wachambuzi mbali mbali wamekuwa wakimuongelea Pogba,na wote kelele zimekuwa zile zile kuhusu pesa aliyosajiliwa na kiwango anachoonesha, lakini mara zote kocha wake Jose Mourinho amekuwa ndio mtetezi pekee wa kiungo huyo wa Kifaransa.

Na sasa kwa mara ya kwanza Pogba amesimama mbele ya waandishi wa habari na kuongea kuhusu dau lake na kuwajibu wale wote wanaozungumzia sana kuhusu dau lake, kwanza Pogba ameshangazwa na jinsi watu walivyoacha mambo mengi na kumuangalia yeye tu na kuhoji kuhusu ufungaji kanakwamba yeye ni mshambuliaji.

“Watu wananiangalia mimi tu na kuanza kunihukumu kwanini sifungi na mambo mambo mengine, mimi ni kiungo lakini kama ningekuwa ninafunga wasingeongea lolote, ona wengine wanazungumzia kuhusu dau langu la usajili lakini usajili ni jambo lingine na uwanjani ni lingine” alisema Pogba.

Pogba alimalizia kwa kusema kwamba yeye anafanya kazi iliyomleta Old Trafford na kazi yenyewe ni kucheza kiungo na sio mshambuliaji, ila akitengeneza nafasi na watu hawafungi hilo sio jukumu lake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.