Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o Yazua Wazo la Filamu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o Yazua Wazo la Filamu

Picha ya Rihanna na Lupita yazua mjadala wa kutengezwa kwa filamu

Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni filamu hatua ambayo imewashinikiza nyota hao kujitokeza na kusema ndio wana mpango huo.

Picha hiyo ya 2014 ya mitindo ilisambazwa na mashabiki wengi na sasa Rihana amesema kuwa ana mpango kama huo katika mtandao wake wa Twitter.

Mashabiki wamependa sana wazo hilo.

Lupita naye alijibu katika mtandao wa Twitter akisema mimi naunga mkono pendekezo hilo iwapo umeunga mkono.

Zaidi ya mashabiki 200,000 walilipenda chapisho hilo la Twitter na mapema siku ya Jumatatu Rihanna alijibu ''I'm Pit'z''-jina la utani katika filamu yake ya Star Wars.
Maoni ya mashabiki kuhusu picha hiyo katika Twitter

Watu wengine 99,000 walilipenda chapisho hilo na sasa nyota hao sasa wameunga mkono pendekezo hilo .
Baadhi ya mashabiki waliopendekeza wazo la filamu ya nyota hao wawili

Wazo la filamu kutokana na picha hiyo lilionekana katika mtandao wa Tumblr wakati picha hiyo ilipochapishwa kwa mara ya kwanza ,lakini sasa wawili hao wamejumuika na sasa inaonekana kwamba mtandao wa Twitter ulitengeza filamu.
Rihanna alijibu kwa kusema kuwa inawezekana

Lakini huku mashabiki wakichangia ni nani anayefaa kupata sifa hizo kwa wazo hilo na kupata faida.

Mashabiki wengi wa Twitter hatahivyo wanegependa wazo hilo kufanikiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.