Picha ya Nywele Asilia za Michelle Obama Yawa Gumzo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha ya Nywele Asilia za Michelle Obama Yawa Gumzo.

Picha ya nywele asilia za bi Michelle Obama yazua hisia mitandaoni

Picha iliomuonyesha mke wa aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama akiwa amezifunga nywele zake nyuma, badala ya alivyokuwa akitengeza nywele zake wakati akiwa mke wa kwanza wa taifa la Marekani katika kipindi cha miaka minane katika ikulu ya Whitehouse imesambazwa sana katika mitandao ya kijamii.

Ujumbe wa Twitter uliochapisha picha ya Michelle Obama umesambazwa zaidi ya mara 30,000.

Haijulikani ni lini ama wapi picha hiyo ilipigwa ,lakini mumewe Barrack Obama anaandika kumbukumbu ya wakati alipokuwa rais katika eneo la Tetiaroa, kisiwa kilichopo kusini mwa Pacific kilichomilikiwa na Marlon Brando, kulingana na gazeti la Washington Post.

Nywele zimekuwa swala la kisiasa barani Afrika miongoni mwa jamii za watu weusi.

Mwandishi wa vitabu nchini Nigeria Chimamanda Ngozi Adichie amesema kuwa iwapo Bi Michelle Obama alikuwa na nywele asili, Barrack Obama asingeebuka mshindi.

Kemikali za nywele ambazo hunyorosha nywele zimekuwa na umaarufu kwa miaka mingi.

Lakini huku mbinu hiyo ya kuweka nyewle ikionekana kuwa ya kitaalam ,wengine wanasema sio ya Kiafrika.

''Kunyorosha nyewle ni sawa na kuwa jela, bi Adichie aliandika. Ni kama mfungwa. Nywele zako zinakutawala''.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.