Mwanaume aliyefanya mauaji huku Akionyesha Live Marafiki zake Kupitia Facebook asakwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwanaume aliyefanya mauaji huku Akionyesha Live Marafiki zake Kupitia Facebook asakwa

Steve Stephens muuaji anayesakwa Marekani

Polisi katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanamtafuta mtu anayedaiwa kufanya mauaji,huku akionyesha moja kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.

Maofisa katika mji wa Cleveland wamesema kuwa Steve Stephens anaonekana akionyesha moja kwa moja mauaji wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima kupitia Facebook.

Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amemtaka Stephens ajisalimishe mwenyewe.

Williams alisema kuwa mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni kwake.

Polisi wanasema hawajapata ushahidi madai ya Stephen kuwa amewauwa watu kumi na mmoja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.