Mvua yaacha wanafunzi 150 bila madarasa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mvua yaacha wanafunzi 150 bila madarasa

SHULE YA SEKONDARI NEW KIOMBOI.

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa takribani nusu saa, imeezua paa za majengo ya Shule ya Sekondari New Kiomboi iliyopo wilayani hapa na kusababisha zaidi ya wanafunzi 150 kukosa vyumba vya kusomea.

Wanafunzi hao kwa sasa wanatumia majengo mawili ya vyumba vya maabara vya shule hiyo.

Mkuu wa shule hiyo, Lameck Ayeiko, alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki.

Aidha, Ayeiko alisema mvua hiyo pia ilisababisha pia ofisi ya mkuu wa shule na za walimu kuezuliwa paa na kujaa maji ndani ya vyumba vya ofisi hizo.

Kwa mujibu wa Ayeiko, zaidi ya Sh. milioni 20 zinahitajika kurudisha majengo hayo katika hali ya kawaida.

“Ili kurudisha yale majengo katika hali yake ya awali, zilikuwa zinahitajika Shilingi milioni 13,648, lakini kuboresha madarasa yale yakae vizuri, kulikuwa kunatakiwa kuwa na ongezeko la kama Shilingi milioni 6,511,000, zote kwa jumla ni zaidi ya Shilingi milioni ishirini,” alisisitiza Mkuu huyo wa shule.

Alisema baada ya tukio hilo, walifanya mkutano wa hadhara kwa kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na kukubaliana kuwa kila mzazi achangie Sh. 10,000.

Ayeiko alisema zaidi ya Sh. 500,000 zilipatikana papo hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya, Emmanuel Luhahula, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

Kihaula alisema baada ya kufanyika tathmini ya uharibifu huo, walibaini zinahitajika zaidi ya Sh. milioni 20 ili kurejesha majengo hayo katika hali yake ya kawaida.

Naye Kkaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mariether Kasongo, alisema kati ya Sh. milioni 30 na milioni 35, zinahitajika kukarabati majengo yaliyoathirika kutokana na mvua hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.