Muuaji Aliyeonekana Akiua LIVE Kupitia Facebook Nae Ajiua. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Muuaji Aliyeonekana Akiua LIVE Kupitia Facebook Nae Ajiua.

Mahusiano na madeni kwenye mchezo wa kamari yalimsukuma Stephens kutekeleza mauaji.

Polisi nchini Marekani wamesema mtu ambaye alifanya mauaji kisha kutuma video ya mauaji hayo katika mtandao wa Facebook amejiua mwenyewe.

Wamesema Steve Stephens alijiua wakati maafisa wa polisi walipolikaribia Gari lake walipokuwa wakimkimbiza takribani kilomita 150 kutoka Cleveland, Ohio, eneo la mauaji yaliyofanyika jumapili.

Picha za video za babu akipigwa risasi zilisalia kwenye mitandao ya kijamii kwa saa mbili bila kuondolewa.

Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg, alieleza maskitiko yake kwa ndugu na akaahidi kuwa kampuni itafanya kila linalowezekana kuzuia jambo kama hilo kuwekwa tena mtandaoni.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.