Mourinho ajinadi kwa Luke Shaw - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mourinho ajinadi kwa Luke Shaw


Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa Luke Shaw alitumia mwili wake lakini ubongo wa Mourinho katika mechi kati ya Manchester United na Everton, ambayo ilisha kwa sare ya 1-1.

Shaw ambaye ana umri wa miaka 21, alicheza mara ya kwanza tangu Januari na ilikuwa penalti iliyotokana na mkwaju wake ambapo Zlatan Ibrahimovic alifunga.

“Alikuwa mbele yangu na nilikuwa nikimfanyia kila uamuzi” Mourninho alisema hayo baada ya mechi kumalizika

Shaw ndiye alikuwa mchezaji mdogo pekee kutoka Manchester aliyetengwa kando na Mourinho baada ya United ilitoka bao sare kwa mara ya tisa nyumbani katika ligi msimu huu.

Ibrahimovic ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu bado hajaamua iwapo atasalia kubaki Old Trafford msimu ujao.

“Bado tunajadiliana, tungoje kuona matokeo, bado nipo wazi na hakuna lolote limetendeka bado”, Ibrahimovic ambaye ana miaka 35 alieleza televisheni ya manchester united.

“Nilikuja hapa bila Ligi ya Mabingwa, haikuwa timu ambayo ilitarajiwa kushinda, lakini bado nilikuja na nikasaidia nilivyoweza ili kuiimarisha, kwa hivyo tungojee kuona matokeo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.