Mb Doggy Awachana Kina Diamond, Kiba. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mb Doggy Awachana Kina Diamond, Kiba.

MSANII mkongwe kwenye Bongo Fleva, aliyewahi kutamba na ngoma za Latifa, Si ulinambia, Mapenzi Kitu Gani na nyingine nyingi, Mbwana Ali ‘Mb Dogg’ amesema ujio wake mpya anaojiandaa kuutoa hivi karibuni utawadhihirishia mashabiki wa muziki nchini kuwa yeye ndiye mfalme wa Bongo Fleva na si mahasimu wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wala Ali Salehe ‘Ali Kiba’.

Akipiga story na Uwazi Showbiz, alisema sababu za kupotea kwenye gemu kwa miaka mingi si kwamba hawezi au alishindwa kuendana na kasi ya vijana walioibuka na kufanya vizuri lakini ni kwa sababu za kimaisha na sasa amejipanga vyema kurudi kwa kishindo.

“Mashabiki wa muziki nchini wanaelewa Mb Dogg ni nani, mimi ndiye mfalme wa Bongo Fleva, nilikuwepo kabla ya akina Diamond na Kiba hawajaanza kuimba, sasa mwenye nyumba karudi na wapangaji wakae tayari, ujio wangu unaitwa Mabinti nimefanyia pale kwa Man Walter,” alimaliza Mb Dogg.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.