Man United yapewa Wababe Wa Samatta Nusu Fainali Ulaya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United yapewa Wababe Wa Samatta Nusu Fainali Ulaya

TIMU ya Manchester United ya England itamenyana na Celta Vigo ya Hispania katika Nusu Fainali Europa League.

Kikosi cha Jose Mourinho kitaanzia ugenini mechi ya kwanza Uwanja wa Balaidos Mei 4 na marudiano yatafuatia Old Trafford Mei 11.

Katika Nusu Fainali nyingine, Ajax ya Uholanzi itamenyana na Lyon ya Ufaransa na mchezo wa kwanza utafanyika Amsterdam.

Man United haijawahi kukutana na timu hiyo ya Hispania hapo kabla kwenye mashindano yoyote, lakini wanajiona bora kuliko Celta iliyo katikati ya msimamo wa La Liga.

Celta Vigo ndiyo imehitimisha safari ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta katika michuano ya Ulaya baada ya kuifunga KRC Genk kwa jumla ya mabao 4-3 wakishinda 3-2 kwenye mchezo wa kwanza Hispania kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena katika mchezo wa marudiano.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.