Man United kuikabili Man City bila Pogba, bila Zlatan, bila Rojo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United kuikabili Man City bila Pogba, bila Zlatan, bila Rojo.

Sahau kuhusu majeraha ya Smalling na Phill Jones waliyoyapata wakati wa kambi ya timu ya taifa ya Uingereza lakini majeruhi ndani ya United wanazidi kumiminika.

Tayari Zlatan Ibrahimovich yuko nchini Marekani kwa ajili ya upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya klabu ya Ubelgiji ya Anderlchelt.

Marcos Rojo naye aliumia katika mchezo huo wa Europa lakini kuna jipya, Paul Pogba hatakuwepo katika mchezo mkubwa kwa Manchester dhidi ya majirani zao City.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema majeruhi aliyopata Pogba katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Burnley utamfanya asiwepo katika Manchester Derby.

Jose Mourinho amesema kutokuwepo kwa Pogba hakuwaumizi sana na wanaamini atarudi siku nyingine na kwa sababu hayupo inabidi wapambane na walichonacho.

Mechi kati ya United na City ni ngumu sana na inavuta hisia za wengi lakini pia klabu hizo mbili zinapigana vikumbo kuingia top four ya ligi na hii inaufanya mchezo huo kuwa mgumu zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.