Man United bado sana - Mourinho - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United bado sana - Mourinho

Jose Mourinho amesema lengo lake la kutegeneza kikosi bora cha Manchester United “ipo mbali” kufikia malengo yake pamoja na kutumia pauni 149 milioni kusajili.

Bosi huyo wa Old Trafford anataka apewa fedha nyingine za kununua wachezaji, akidai klabu yake ilipoteza nafasi ya kufanya hivyo katika uhamisho wa Januari.

Mourinho anakata mshambuliaji mpya wa kiwango cha Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, pamoja na viungo wawili wa kumsaidia Paul Pogba, na mabeki wawili wa pembeni.

Usajili wake huo utaighalimu klabu yake zaidi ya Pauni 200 milioni, utaifanya kutimua zaidi ya Pauni 350 milioni kwa mwaka.

Akizungumzia mwenendo wa timu yake katika nafasi ya sita, kocha huyo alisema: “Tunahitaji kipindi cha usajili tena.”

Wakati alipoulizwa kuhusu ubora wa kikosi chake ndiyo kile alichokuwa anakitaka, alijibu: “Bado. Tupo nyuma sana. Tunahitaji dirisha moja la usajili.

“Hatukutumia usajili wa dirisha dogo. Ni wazi tunahitajio kujimalisha zaidi. Tunatakiwa kuimarisha kikosi chetu.”

Wakati bei ya Griezmann ni pauni Pauni 86 milioni, pia Mourinho anamtaka beki wa kulia wa Monaco, Djibril Sidibe (22mil) na Benjamin Mendy (15mil).

Katika kuimarisha kiungo anamtaka nyota wa Tottenham, Eric Dier mwenye thamani ya Pauni 40 milioni pamoja mchezaji wa Monaco Tiemoue Bakayoko (35mil).    

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.