Mahakama yamwagiza Manji kufika kortini - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mahakama yamwagiza Manji kufika kortini

MFANYABIASHARA YUSSUF MANJI.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeagiza mfanyabiashara Yussuf Manji kufika mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili ya kutumia dawa za kulevya.

Agizo la mahakama lilitolewa baada ya upande wa utetezi jana kudai kuwa Manji ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu mgonjwa.
Kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Wakili wa Serikali, Batlida Mushi, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwamba mshtakiwa hakuwapo mahakamani.

 Upande wa utetezi ulidai kuwa mshtakiwa ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, anasumbuliwa na maradhi ya moyo.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkeha aliagiza kuwa tarehe ijayo mshtakiwa afike mahakamani kusikiliza kesi yake. Alisema kesi hiyo itatajwa tena Mei 19, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi,  Manji ambaye pia ni, Diwani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mbagala Kuu, anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya.

Ilidaiwa kuwa  kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View, jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya  aina ya Heroin. Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.