List ya Miji yenye watu Wengi zaidi Duniani kote. Tanzania Je? soma habari hii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

List ya Miji yenye watu Wengi zaidi Duniani kote. Tanzania Je? soma habari hii

Hivi uliwahi kujiuliza nchi yako ni yangapi katika nchi zenye watu wengi zaidi. Ama umewahi kubashiri mwenyewe nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi.

Bongoswaggz inakumalizia mzozo huo na inakupa list kamili ya miji inayoongoza kwa watu wengi zaidi duniani kote.


Namba 10.

Buenos Aires- Argentina.
Huu ni mji wenye wakazi wapatao milioni 12, Unaopatikana Amerika Kusini. Wakazi wengi (97%) wa mji huo wana asili ya Ulaya na Mashariki ya Kati, hasa Italia (55%) na Hispania.Namba 09.Bu
Kalkutta-Uhindi .(India)
Mji huo una wakazi wapatao milioni 13, na unapatikana Bengali Magharibi katika bara la Asia.Namba 08.
Los Angeles – Marekani.
LA ni kati ya miji maarufu duniani kwa starehe, na una jumla ya wakazi milioni 13. Inasemekana kua mji huu hupendelewa zaidi na watu wanaopenda starehe.Namba 07.
Lagos – Nigeria .
Mji huu upo Barani Afrika, na ni wenye jumla ya wakazi milioni 13. Lagos ni mji mkuu wa nchi ya Nigeria.Namba 06.
Shanghai-China.
Nchi ya china inaoongoza kwa wafanya biashara duniani. China, inyapatikana katika bara la Asia ya Mashariki,ni nchi yenye watu wengi duniani. Mji wa Shanghai una jumla ya watu milion 14.Namba 05.
New York City – Marekani.
Jiji hilo anakotokea rais wa Marekani, Donald Trump,lina wakazi milioni 17. Nchi ya Marekani ina ukubwa wa kilometa mraba 9,826,675 na lipo katika bara la Amerika Kaskazini kati ya Canada upande wa kaskazini na Mexico upande wa kusini.


Namba 04.
São Paulo – Brazil .
Brazil ni nchi kubwa ya Amerika ya Kusini na pia ni nchi yenye wakazi wengi. Ukubwa wa nchi hiyo ni karibu nusu ya bara lote. Mji wake wa Sao Paulo una wakazi milioni 18.Namaba 03.
Mumbai – Uhindi(India)
Mji huu ulianzishwa kwenye kisiwa kilichopo karibu sana na bara. Kitovu kipo kwenye rasi inayoelekea katika Bahari ya Hindi. Kisiwa kilinunuliwa na Wareno mwaka 1534 nao Wareno waliwakabidhi kisiwa kwa Uingereza 1661, Mji wa Mumbai una wakazi milioni 18.


Namba 02.
Mexico City – Mexico
Mji wa Mexico pia ni mkoa wa kujitegemea, huitwa mara nyingi na Wamexiko wenyewe “Mexico DF” au kwa kifupi “DF” (DF = Distrito Federal, Mkoa wa Shirikisho), lakini tangu mwaka 2016 unaelekea kujitegemea zaidi kiutawala. Una wakazi milioni 18.Namba 01.
Tokyo – Japani.
Japani ni kati ya nchi zilizoendelea hapa duniani kwa upande wa sayansi, teknolojia na uchumi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda. Mji huo una wakazi milioni 28.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.