kwa mara ya kwanza Nape bungeni auliza haya kama mbunge. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

kwa mara ya kwanza Nape bungeni auliza haya kama mbunge.

Kwa mara ya kwanza aliyekuwa Waziri wa habari Nape Moses Mnauye asimama bungeni kama mbunge na kuuliza swali kwa waziri wa uchukuzi na mawasilioano.

Nape Mnauye alisimama kuuliza swali la nyongeza ambapo aliitaka serikali kuweka mipango yao ya kufanya upanuzi wa Barabara na Reli.

Nape alitaka Serikali ielekeze mipango yao mapema katika upanuzi wa miundombinu iliyokaribu na makazi ya wananchi na kutowaweka wananchi njia panda katika kuyaeneleza makazi yao.
Akitoa mfano jimboni kwake Mtama amesema kuwa wananchi wapo njia panda kujua hatma yao.

Swali hilo lilijibiwa  na Naibu wa Waziri wa wizara hiyo Mhandisi Edwin Ngonyani wizara ya Uchukuzi na Mawasilioa na Kujibiwa na naibu Waziri wa wizara hiyo
 Waziri Ngonyani alijibu kuwa  Serikali imeweka alama kutoka mita 30 za kila upande wa barabara kuonesha hifadhi ya barabara

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.