Kwa Lugha Yake Ya Mwili Anaongea Mengi Kuliko Anavyomaanisha, Jifunze Kuielewa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kwa Lugha Yake Ya Mwili Anaongea Mengi Kuliko Anavyomaanisha, Jifunze Kuielewa.


Tofauti na wanawake, wanaume huwa tunaongea tunachokimaanisha na tumaanisha tunachokiongea, wanawake wapo tofauti sana na asilimia 80% ya wanachokiongea huwa akimaanishi kile wanachokitamka, anaweza kukwambia sitaki kumbe anamaanisha anataka na anapendezwa na unachokifanya, ndo maana ili kuelewa mwanamke anachokimaanisha ni muhimu katika hali ya juu sana kujua lugha na pozi zake za mwili ili ujue anachotaka na kumaanisha.

Wanawake muda wote hutoa ishara ya mwili ya kile wanachokitaka, na iwapo ukizielewa na kuwa mkufunzi katika kuzijua na kuzielewa, utakuwa na silaha kubwa ya kujua macho yake na mwili wake unavyoongea kabla hata hajafungua kinywa chake.

Mapozi.

Wanawake ambao huitaji akili ya mwanaume iwepo kwao huwa ni rahisi kuwagundua hata kama ni katikati ya umati, mapozi na lugha yao ya mwili huwa inakuita iwapo wewe ni mjuzi wa lugha yao ya mwili, kwa mwanzo hujiinamisha kidogo kwenye uelekeo wa mwanaume ambae amevutika nae, na mara kwa mara hukutanisha macho. Hucheka mara kwa mara zaidi ya kawaida bila ya kuwa mshikaji anaeongea nae ni mcheshi au vipi, hutafuna midomo yao na nyuso zao zipo katika hali ya udadisi.

Wanawake wanaojiweka katika hali ya utongozwaji huwa katika hali ya kutojiamini sana, kwa mfano huchezea vidole vyao, nywele, mikufu na kadhalika, hii hutokana na kuwa na wasiwasi mwingi na moyo yao kuwa katika mapigo yaendayo kasi, na huitaji kufanya vitendo vya kujitulizisha akili.

Jinsi ya kufanya; Kama mwanamke huyo yupo katika uelekeo wako na anaonyesha tabia hizi kama tulivyoorodhesha hapo mwanzo, inatakiwa ujipe uhakika mkubwa wa maongezi na utongozaji kwenda vizuri, hivyo msogelee kwa pozi na fanya yako kwa staili.

Matamanio.

Matamanio huwa na ishara sawa na za kutaka kutongozwa ila hizi zinakuwa za matamanio ya kumaliza haja ya mwili, Jaribu kumfikilia Shilole kwenye video zake za mziki na utapata wazo nazungumzia nini, anakuwa anakutanisha macho zaidi katika hali ya kurembua, mapozi yanakuwa katika hali ya matamanisho zaidi, hipsi na matiti yanakuwa yamejitokeza zaidi, na mara nyingi tabia hizi hutokea katika sehemu zilizojificha au zenye hali ya kimahaba zaidi kama kwenye klabu.

Angalia iwapo kama anapumua kwa uzito zaidi maana hii humaanisha tamanio, kwa mfano anapumua pumzi ndefu zaidi ukimsogelea karibu, au ikitokea mguso kati yako na yeye ? Anaweza jaribu kukugusa katika hali ya kukupapasa.

Jinsi ya kufanya; Yupo tayari, nawe mjibu kwa pozi na taratibu, jiachie taratibu ukimjibu mapozi yake, muangalie kwa husuda na kutanisha macho na tengeneza sababu za kumgusa, mwanzo wa kumgusa mguse taratibu na endeleza mashambulizi iwapo asipojitoa katika hali hio.

Wanawake wengine hawajielewi kile wanachokihitaji, kwa mfano anaweza kuwa amependezwa na wewe ila akawa anakujibu katika hali ya ukali, hii inakuwa ni hali ya kutojionyesha anajirahisisha kwako, kwa hio japo anafanya hali ya ukali ila moyoni anakuwa katika hali ya kukukubali tayari.

Kumbuka, lugha ya mwili, mapozi na muonekano huongea zaidi ya maneno, mchunguze mapozi yake kwa umakini, mwanamke akipendezwa nawe anakusaidia katika kumtongoza, mapozi yake yatakuita, maneno yake yataendana na stori zako, ikitokea fanya kama unavyopaswa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.